Askofu wa jimbo Katoliki la Shinyanga mhashamu LIBERATUS SANGU amewaomba waamini wa jimbo la Shinyanga kuungana na wenzao wa jimbo la Tunduru Masasi kusali kumwombea askofu wa jimbo hilo Mhashamu CASTORY MSEMWA ambaye amefariki dunia jana huko nchini Oman.
Akitangaza rasmi taarifa za kifo hicho kwa waaminimi wa jimbo la Shinyanga kupitia misa maalum iliyofanyika leo katika parokia ya Mipa, askofu Sangu amesema kifo cha askofu MSEMWA ni pigo kubwa kwa kanisa la Tanzania hivyo Wanashinyanga hawanabudi kusali kuliombea jimbo la TUNDURU MASASI ili lipate mchungaji mwingine mapema
Marehemu askofu CASTORY PAUL MSEMWA amezaliwa mnamo mwaka 1955 katika kijiji cha Kitulira parokia ya Matola jimbo katoliki la Njombe ambapo baada ya kumaliza masomo yake ya falsafa na Theolojia alipewa daraja takatifu la upadre mnano Juni 7 mwaka 1987 huko jimboni Njombe.
Alipewa daraja takatifu la uaskofu mnamo Januari 30 mwaka 2005 na kuwekwa wakfu kuwa askofu wa jimbo la TUNDURU MASASI mnamo Agosti 25 mwaka 2005.
Amefariki dunia jana saa saba mchana mjini Muscat nchini Oman akiwa safarini kuelekea nchini India kwa matibabu.
Mungu ailaze mahali pema mbinguni roho ya marehemu askofu CASTORY MSEMWA.