Bugisi T.C

HISTORIA FUPI YA BUGISI TRAINING CENTRE

Shule ya Bugisi Training Centre, ilianzishwa na Masister wa O.L.A ( Our Lady of Apostles) mnamo mwaka 1996.  Hii ilikuwa na malengo ya kukidhi mahitaji ya watu wa mazingira ya karibu na chuo.  Ilikuwa imelenga kwa akina mama na wasichana wa Parokia ya Bugisi kufika kujifunza maarifa ya nyumbani kama (ushonaji, upishi, chakula bora, mipangilio ya bajeti kwa mahitaji ya nyumbani n.k.)

Baada ya muda, watu kutoka nje ya parokia hii walianza kuomba nafasi.  Hivyo watu walianza kukifahamu vizuri chuo chetu.

UJENZI WA BWENI LA WANAFUNZI.

Shule ilianzisha mipangilio ya kujenga bweni la wanafunzi wa kike kufikia mwaka 2002,  shule ilikamilisha ujenzi wa bweni walianza kutumia na mpaka sasa wanafunzi 80 wa kukaa bweni.

USAJILI WA CHUO.

Mwaka 2002 shule iliomba kusajiliwa chini ya VETA (Vocational Education and Training Authority)  na mwaka 2003 wanafunzi walishiriki mitihani ya VETA ambayo ni TRADE TEST (Upishi na Ushonaji) na NABE (English na Typing).

Mwaka 2004 VETA walifika kufanya ukaguzi ili wafanyie usajili shule.  Pia chuo kilipata mwaliko wa kushiriki maonyesho ya VETA Kanda ya Magharibi, chuo chetu kilikpata nafasi ya nne (4) kati ya vyuo 32.

LENGO LA SHULE.

Lengo la shule hii ni kuwafundisha wasichana kuhusu maarifa kiuchumi kataka maisha yako ya baadaye na familia zako ili kuwawezesha kutumia rasilimali walizonazo katika mazingira yao ili ziweze kuwasaidia kuishi maisha bora.

Chuo kiliamua kuwapa wanafunzi nafasi ya kusoma miaka mitatu, ili kuwasaidia wanafunzi kukamilisha madaraja yote ya mitihani ya VETA.

MAFUNZO YA COMPUTER.

Chuo kina toa nafasi kwa wanafunzi kushiriki masomo ya computer kama ziada kwa wanafunzi ambao wana uwezo wa kutumia lugha ya kiingereza hasa waliomaliza kidato cha nne(IV). Somo hili linaendeshwa nje ya vipindi vya shule na ada yake ni tofauti na gharama ya ada ya shule.

CHUO KINAFUNDISHA KOZI ZIFUATAZO:-

A)  SECRETARIAL COURSE.

Kozi hii inafundishwa kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne na masomo kama

ifuatavyo:- Computer, Typing, French, Office Practice, Commerce, English,

Social Skills,Entrepreneurship, Secretarial Duties e.t.c.

B)  FOOD PRODUCTION.

Kozi hii watachukua walimaliza kidato cha IV masoma kama ifuatavyo:- Food

Production, English, Social Skills, Life skills, Computer, Entrepreneurship, French,

Food human nutrition e.t.c.

C)  SHORT-COURSE.

Mafunzo haya ni kwa wanafunzi walioshindwa kumaliza darasa la saba, walio-

maliza darasa la saba na ambao hawana uwezo kwenye masomo mengine, itawabidi

masomo haya:- Ushonaji, Upishi, Chakula bora, English course, mambo ya maisha,

Art/craft, Entrepreneurship e.t.c.