Askofu wa jimbo katoliki la shinyanga mhashamu LIBERATUS SANGU amekitangaza rasmi kigango cha kitangili kilichopo katika parokia ya buhangija mjini shinyanga kuwa parokia teule ambayo itakuwa chinbi ya usimamizi wa mtakatifu rosa wa lima.

Tamko la kukitangaza kigango hicho kuwa parokia teule amelitoa siku ya jumapili tarehe 05th, October  mara baada ya adhimisho la misa takatifu ya jumapili ambayo imefanyika katika kanisa la mtakatifu rosa wa lima parokia teule ya kitangili

Kufuatia tamko hilo askofu sangu amemteua padre RAFAEL ISLAHIM kuwa msimamizi wa parokia hiyo teule.

Parokia teule ya kitangili ambayo inakadiriwa kuwa na waanimi zaidi ya elfu mbili  inatokana na kumegwa kwa eneo la parokia ya buhangija ambayo ni moja ya parokia kongwe katika jimbo la shinyanga.

Jimbo la shinyanga kwa sasa lina jumla ya parokia kamili 32 na parokia teule sita.