Maandamano ya Misa maalumu ya utolewaji wa daraja takatifu la Upadre kwa Mashemasi sita wa Jimbo katoliki la Shinyanga iliongozwa na Mhashamu Polycarp Kadinali Pengo.

Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo na Mhashamu Baba Askofu Liberatus Sangu wa jimbo la Shinyanga wakiingia katika kanisa kuu la Mama mwenye huruma kwaajili ya adhimisho la Misa maalumu ya utolewaji wa daraja takatifu la Upadre kwa Mashemasi sita wa Jimbo.

Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo akiendelea na Misa ya Upadirisho ya Mashemasi sita wa Jimbo la Shinyanga.

Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo akiendelea na Misa ya Upadirisho ya Mashemasi sita wa Jimbo la Shinyanga.

Mkurugenzi Msaidizi wa Miito Jimbo Katoliki la shinyanga Padre Deograthius Ntindiko akiwaita na kuwatambulisha mbele ya Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo Mashemasi sita wa Jimbo kwaajili ya kupewa Daraja takatifu la Upadre.

Mashemasi wakijongea mbele ya Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo kwaajili ya ibaada ya utolewaji wa daraja takatifu la Upadre.

Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo akitoa homilia kwa Mashemasi kabla ya kuwapa daraja takatifu la upadre.

Mashemasi wakiwa mbele ya Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo ,(kushoto) ni Shemasi Martine Masanja wa parokia ya Mipa,Richard Masunga wa parokia ya Malili,Peter Mkunya wa parokia ya Malampaka,Gregory Samike wa parokia ya Salawe,Peter Tungu wa parokia ya Mwanhuzi,na Martine Jilala wa parokia ya Mipa.

Mashemasi wakiwa wamejilaza kifudifudi wakati wa sala ya Litania ya watakatifu wote.

Mashemasi wakiwa wamejilaza kifudifudi wakati wa sala ya Litania ya watakatifu wote.

Mashemasi wakiwa wamepiga magoti kwaajili ya kuwekewa mikono ishara ya kumpokea Mungu roho Mtakatifu.

Mashemasi wakiwekewa mikono na Mapadre ishara ya kumpokea Mungu roho Mtakatifu.

Misa ya Upadirisho ikiendelea katika kanisa kuu la Mama mwenye Huruma Ngokolo mjini Shinyanga.

Maparoko wa parokia walizozaliwa wakiwavisha Mavazi rasmi ya kipadre baada ya kupewa daraja takatifu la upadre.

Wakipongezwa baada ya kupewa daraja takatifu la upadre.

Wakiwa na Mavazi rasmi ya kipadre baada ya kupewa daraja atakatifu la upadre na Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo.

MMoja wa Mapadre wapya Padre Richard Masunga akipakwa mafuta matakatifu ya krisma viganjani kwaajili ya kuwatakasa watu.

Padre mpya Peter Tungu akikabidhiwa Mkate na Divai ambavyo atavitumia kuadhimisha misa takatifu.

Mwadhama Polycarp kadinali pengo na Mhashamu Liberatus Sangu wakiwapongeza Mapadre wapya mara baada ya kupewa daraja takatifu la upadre.

Mapadre wakiwapongeza Mapadre wapya mara baada ya kupewa daraja takatifu la Upadre

Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo akiwapa wosia kuhusu majukumu wanayokwenda kuyafanya Mapadre wapya mara baada ya kuwapa daraja takatifu la Upadre.

Waamini wakiwa katika Misa ya Upadirisho.

Baadhi ya viongozi wa Serikali akiwemo mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack na mkuu wa Wilaya yaShinyanga Jasinta Mboneko wakiwa ksatika Misa ya Upadrisho.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack akitoa Salamu kwaniaba ya Serikali katika Misa ya Upadrisho.

Mkuu wa Mkoa Zainabu Telack akimpongeza Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo mara baada ya kuwapa daraja takatifu la Upadre Mashemasi sita wa jimbo (kulia )Mhashamu Baba Askofu Liberatus Sangu wa Jimbo la Shinyanga.

Makamu wa Askofu wa jimbo la Shinyanga Padre kizito Nyanga akishikana mkono na Mwadhama Polycarp kadinali Pengo katika misa ya upadrisho.

Mwadhama Polycarp Pengo akiwashukuru wanajimbo ;la Shinyamnga kwa kupata Mapadre wapya sita kwa mpigo.

Mapadre wapya wakiwabariki Mwadhama Polycarp kadinali Pengo na Mhashamu baba Askofu Liberatus Sangu.

Mapadre wapya wakiwabariki waamini.

Mwadhama Polycarp kadinali Pengo akihitimisha adhimisho la misa takatifu ya utolewaji wa daraja takatifu la Upadre.

Mwadhama Polycarp kadinali Pengo na Mhashamu Liberatus Sangu wakiwa katika picha ya pamoja na Mapadre wapya sita wa Jimbo la Shinyanga.

Mwadhama Polyacarp kadinali Pengo katika Picha ya Pamoja na Mwenyeji wake Mhashamu Baba Askofu Liberatus Sangu wa Jimbo la Shinyanga.

Mwadhama Polycarp kadinali Pengo na Mhashamu Liberatus Sangu wakiwa katika picha ya pamoja na Mapadre wapya sita wa Jimbo la Shinyanga pamoja na baadhi ya Mapadre.

Mwadhama Polycarp kadinali Pengo.

Mwadhama Polycarp kadinali Pengo na Mhashamu Liberatus Sangu wakiwa katika picha ya pamoja na Mapadre wapya sita wa Jimbo pamoja na viongozi wa Serikali ya Mkoa wa Shinyanga .

Baadhi ya walelewa wa Shirika la Kijimbo la Mt.Maria Mama Mwenye Huruma wakiwa katika Misa ya Upadrisho.

Mapadre wapya sita wa Jimbo la Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja.

Mhashamu Baba Askofu liberatus Sangu akimshukuru Mwadhama Polycarp kadinali Pengo kwa kukubali kuwapa daraja takatifu Mashemasi wa Jimbo lake.

Mwadhama akimuwekea mikono Shemasi Martine Jilala.

Padre mpya Martine Masanja akila kiapo cha utii kwa Askofu wa Jimbo la Shinyanga na waandamizi wake kupitia mikono ya Mwadhama Polycarp kadinali Pengo.