Maandamano kuelekea kanisani

Mashemasi wateule Baltazar Zengo kushoto na Mwenzake Patric Ngasa kulia wakiingia kanisani tayari kwa misa ya ushemasi.

Mashemasi wateule wakiwa kanisani.

Mashemasi wateule wakisikiliza homilia wakati ikitolewa na Mhashamu Baba askofu Liberatus Sang wa kwanza kulia ni Placido Nkalangi wa parokia ya Ngokolo,katikati Balatazar Zengo wa parokia ya Nyalikungu na Kushoto ni PatricK Ngasa Dogani wa parokia ya Nyalikungu.

Mashemasi wateule wakithibitisha nia yao ya kupewa daraja la ushmasi mbele ya Mhashamu baba askofu

Mhashamu Baba askofu akiwahoji mashemasi wateule ju ya nia yao ya kupewa daraja la ushemasi

Shemasi mteule Patrick Ngasa Dogani akiahidi utii mbele ya Mhashamu Baba askofu.

Mashemasi wateule wakiwa majilaza kifudifudi wakati sala ya litania ya watakatifiu wote ikiendelea

Mhashamu Baba askofu akiiongoza sala maalum ya kuwaweka wakfu kuwa mashemasi mashemasi hawa wateule

Mashemasi baada ya sala ya kuwaweka wakfu

Mhashamu Baba askofu akimwekea mikono shemasi Baltazar Zengo

Mhashamu Baba askofu akimwekea mikono shemasi Patrick Ngasa Dogani

Mhashamu Baba askofu akikamilisha taratibu za kuwaweka wakfu