Maandamano ya kuingia Kanisani katika Misa ya Utoaji wa Daraja Takatifu la Ushemasi kwa Mafrateri Peter Tungu, Peter Lyuba, Martine Masanja, Martine Jilala, Gregory Samike na Richard Masunga katika Sikukuu ya Kuongoka kwa Takatifu Paul Mtume 25 Januari, 2019

Mhashamu Askofu Liberatus Sangu wa Shinyanga akitoa homiliia katika adhimisho la Ekaristi Takatifu kabla ya kutoa Daraja Takatifu la Ushemasi kwa Mafrateri sita (6) katika Kanisa Kuu Mama Mwenye Huruma Ngokolo Shinyanga tarehe 25.01.2019

Mashemasi wateule wakiwa wamejilaza kifudifudi wakati wa Sala ya Litania ya Watakatifu wote wakati wa Misa ya Daraja Takatifu la Ushemasi.

Mhashamu Askofu Liberatus Sangu wa Shinyanga akimkabidhi cheti cha uthibitisho wa kupokea Daraja Takatifu ya Ushemasi Richard Masunga kutoka Parokia ya Yesu Kristo Mfalme, Malili.

Mhashamu Askofu Liberatus Sangu wa Shinyanga akizindua Jubilee ya Miaka 50 ya Utume wa Halmashauri Walei tangu utume huo uanze rasimi nchini. Kama ishara ya uzinduzi huo na ustawi wa Utume wa Walei Askofu Sangu aliwasha mishumaa 32 kwa Parokia zote zilizopo Jimboni hapo.

Mhashamu Askofu Liberatus Sangu wa Shinyanga akibeba mshumaa muda mfupi kabla ya kuzindua Jubilee ya Utume wa Walei ambapo utume huo unaadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa nchini Tanzania.

Mashemasi wapya wakiwa katika picha ya pamoja na Mhashamu Askofu Sangu mara baada ya kupewa Daraja hilo katika Kanisa Kuu Mama Mwenye Huruma Ngokolo jimboni Shinyanga.

Askofu Sangu katika picha ya pamoja na Maklero mara baada ya Misa ya utowaji wa Daraja la Ushemasi katika Sikukuu ya Kuongoka kwa Mtakatifu Paulo Mtume, Januari 25, 2019

Askofu wa jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu akiwa pamoa na vijana wa Mwaka wa nyumba ya Malezi iliyoko katika Parokia ya Sayusayu wakati viana hao walipohudhuria Misa ya Utowaji wa Daraa Takatifu la Ushemasi kwa Mafrateri sita (6) .